CUF.: WAZIRI MKUU AINGILIE KATI MGOGORO WA UMEYA KATIKA JIJI LA TANGA

Chama cha wananchi CUF Kimemtaka Waziri Mkuu kassim Majaliwa kassim Kuingilia kati Mgogoro wa Umeya katika jiji la Tanga ambao umechukua takriban miezi minne sasa na Kuzorotesha mipango ya maendeleo ya wananchi katika jiji hilo.

Naibu katibu Mkuu wa Chama hicho Magdalena Sakaya akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm amesema Ombi hilo la kuingilia kati Mgogoro huo linatokana na Kushindwa kwa Waziri wa Tamisemi kutatua mgogoro huo licha ya kuahidi kuupatia Ufumbuzi.
Amesema bila kuupatia Ufumbuzi mgogoro huo katika kumpata meya halali anayekubalika hakutakuwa na suluhisho hivyo wananchi wataendelea kukosa huduma muhimu zinazopaswa kutengewa bajeti na manispaa ya jiji hilo.

Aidha Cuf imelilalakikia jeshi la polisi katika jiji hilo kwa kuwakata vingozi na madiwani wa chama hicho akiwemo mgombea wa nafasi ya umeya kwa madai ya kutoa lugha za uchochezi huku pia ikipiga marufuku mikutano ya ndani na hadhara ya chama hicho.
Sakata la Umeya katika jiji la tanga linatokana na Uchaguzi uliofanyika miezi mitatu iliyopita ambapo Mkurugenzi wa jiji hilo alimtangaza mgombea wa Ccm Kushinda nafasi hiyo,huku chama Cuf Kikiwa na madiwani 20 na Ccm madiwani 17.
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment