Kocha wa Yanga Mholanzi Hans van der Pluijm,amesema pamoja na kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini anajivunia kiwango bora walicho kionyesha mbele ya mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika Al Ahly.
Pluijm ameiambia Goal, kilichowaondoa kwenye michuano hiyo ni kukosa bahati lakini walicheza vizuri kwa dakika zote za mchezo na kuwaweka katika wakati mgumu wapinzani wao Al Ahly, waliokuwa nyumbani uwanja wa Borg El Arab Alexandria Misri.Bao la dakika za majeruhi la kiungo Abdallah Said lilikatisha ndoto za vijana wa Jangwani ya kucheza hatua ya makundi na sasa imehamishiwa kwenye michuano yaKombe la Shirikisho
0 comments:
Post a Comment