![]() |
BARCELONA v ATLÉTICO MADRID |
Usiku Mabingwa Watetezi wa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, FC Barcelona wako kwao Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain kucheza na wenzao wa Spain Atletico Madrid kwenye Mechi ya kwanza ya Robo Fainali
Mechi nyingine ya Robo Fainali Siku hiyo hiyo ni huko Munich, Germany wakati Bayern Munich watacheza na Benfica ya Portugal.
Barcelona wanaingia kwenye Mechi hii na Atletico Madrid wakitoka kwenye kipigo kitakatifu cha Jumamosi Uwanjani kwao Nou Camp mikononi mwa Mahasimu wao wakubwa Real Madrid waliowachapa 2-1 kwenye Mechi ya La Liga.
Kipigo hicho kilukuwa cha kwanza kwa Barca katika Mechi 39 chini ya Kocha Mkuu wao Luis Enrique.
Mbali ya hilo, Barca wanatinga kwenye Robo Fainali hii wakiwania kuwa Timu ya kwanza tangu Miaka ya 1990 kuweza kutetea vyema Taji lao la Ulaya ambalo wao walishindwa kufanya hivyo Mwaka 2010 na 2012.
Lakini Wachambuzi wengi, hasa wa huko Spain, wamekuwa na wasiwasi na Barca kwa sasa baada ya kuonekana wakiwa goigoi walipofungwa Juzi na Real.
-Barcelona wameshinda Mechi 6 zilizopita dhidi ya Atletico Madrid lakini katika Mechi yao pekee ya Ulaya, Atletico iliibwaga Barca kwa Jumla ya Bao 2-1 katika Mechi 2 za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Msimu wa 2013/14.
![]() |
Bayern Munich v Benfica |
0 comments:
Post a Comment