Rais wa Sudan Omar al-Bashir ameambia BBC kwamba ataondoka madarakani mwaka 2020 muhula wake wa sasa utakapomalizika.
Bw Bashir pia amekanusha tuhuma kwamba wanajeshi wake wamekuwa wakitekeleza dhuluma kwenye vita vipya dhidi ya wanavijiji weusi katika eneo la Darfur, magharibi mwa nchi hiyo.
Kiongozi huyo anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita.
Bw Bashir amekuwa madarakani tangu 1989. Alishinda uchaguzi mkuu Aprili mwaka jana.
Hata hivyo, wakosoaji wake watasema tayari amewahi kuahidi kungĂatuka awali lakini baadaye akakosa kutimiza ahadi hiyo, mwandishi wa BBC anasema.
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 2.5 milioni wamefurushwa makwao Darfur tangu 2003, zaidi ya 100,000 wakitoroka makwao mwaka huu pekee.
Rais Bashir amesema hakuna haja ya kuwa na walinda Amani wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa kutoa misaada eneo la Darfur.
- Blogger Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment